Katika wiki za karibuni Tanzania inashuhudia ongezeko la matukio ya ajali zilizogharimu maisha ya watu zikitokea ikiwemo ajali ya hivi karibuni iliyotokea katika barabara ya Dodoma Morogoro iliyohusisha Basi na roli na kusababisha vifo vya watu 12 na majeruhi 63, huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa uzembe wa madereva.