JamiiNigeria
Misururu mirefu ya wanunuzi wa mafuta yashuhudiwa Nigeria
31 Mei 2023Matangazo
Matamshi hayo aliyatoa katika hotuba yake ya kwanza alipoapishwa siku ya Jumatatu. Hotuba ya Tinubu alizusha wasiwasi alipotangaza kuwa ruzuku ya mafuta imeondolewa. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Petroli Nigeria, Mele Kyari, amesema ukweli ni kwamba serikali haiwezi tena kulipia ruzuku ya mafuta. Akizungumza jana na waandishi habari, Kyari amesea serikali inahitaji kulipa hadi naira trilioni 2.8 ambazo ni sawa na dola bilioni 6 kwa ajili ya ruzuku. Hata hivyo, amesema mazungumzo mengine yanaendelea ili kuleta unafuu kwa wananchi. Baadhi ya vituo vya mafuta ya petroli tayari jana vilianza kupandisha bei ya petroli, na hadi sasa serikali mpya haijatangaza hatua zozote za kuleta suluhisho kwa watumiaji mafuta.