SiasaNigeria
Niger yapiga marufuku uuzaji wa nafaka nje ya nchi
18 Oktoba 2024Matangazo
Taarifa iliyotolewa na serikali imesema kuwa kiongozi wa kijeshi wa Niger Abdourahmane Tiani amechukua hatua hiyo ili kulinda usambazaji wa soko la ndani na upatikanaji wa kutosha wa bidhaa zinazotumiwa kwa wingi.
Adhabu kwa wale watakaokiuka agizo hilo ni kukamatwa kwa shehena na mashitaka ya jinai.
Niger ni mshirika muhimu wa kikanda wa nafaka kwa baadhi ya majimbo katika taifa jirani la Nigeria. Ingawa vikwazo vilivyowekwa kwa Niger na jumuiya ya kikanda ya ECOWAS viliondolewa mwezi Februari, lakini vimetatiza soko la nchi hiyo huku mfumuko wa bei ukiendelea kuwa juu.