Niger yaliamuru jeshi kuwa kwenye tahadhari kubwa
26 Agosti 2023Kiongozi wa ulinzi amesema tahadhari hiyo inaruhusu wanajeshi kujibu mashambulio wakati wowote ili kuepuka mashambulizi ya kushtukiza.
Jumuiya ya kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS imekuwa ikijaribu kujadiliana na viongozi waliofanya mapinduzi Julai 26, lakini imesema iko tayari kutuma wanajeshi wake kurejesha utawala wa kikatiba iwapo juhudi za kidiplomasia zitafeli.
ECOWAS yakataa kipindi cha mpito cha miaka mitatu Niger
Lakini mkuu wa kamisheni wa Jumuiya hiyo Omar Alieu Touray, hapo jana alisisitiza kuwa ECOWAS haijatangaza vita kwa watu wa Nigerwala hakuna mpango wowote wa kutangaza vita kama inavyodhaniwa kuwa wanataka kuivamia nchi hiyo kijeshi.
Uamuzi wa jumuiya hiyo mwanzoni mwa mwezi Agosti wa kupeleka wanajeshi wake Niger ulizua hofu ya mzozo kutanuka na kuliyumbisha eneo la Sahel linalopambana na uasi.