1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger yafunga anga ikihofia uvamizi wa ECOWAS

7 Agosti 2023

Watawala wa kijeshi nchini Mali wametangaza kulifunga anga la nchi hiyo, huku vijana wakifanya doria sehemu mbalimbali Niamey kufuatia kitisho cha uvamizi wa kijeshi kutoka mataifa wanachama wa jumuiya ya ECOWAS.

https://p.dw.com/p/4UqWN
Niger, Niamey | General Abdourahmane Tchiani bei einer Kundgebung von Anhängern der Putschisten
Picha: Balima Boureima/AA/picture alliance

Hayo ni wakati muda wa mwisho waliowekewa wakuu hao wa kijeshi kumrejesha madarakani rais aliyepinduliwa, Mohamed Bazoum, ukimalizika.

Ufaransa ilisema ingeliunga mkono hatua yoyote ambayo ingelichukuliwa na ECOWAS.

Soma zaidi: Wakuu wa ulinzi wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi, ECOWAS wanakamilisha mipango ya kuingilia kati kijeshi nchini Niger.

Maelfu ya raia wanaounga mkono mapinduzi hayo walikusanyika katika uwanja wa michezo mjini Niamey wakishangilia uamuzi wa jeshi kutokubali shinikizo lolote kutoka nje.

Kutokana na utajiri wake wa urani, mafuta na jukumu lake katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi, Niger ina umuhimu mkubwa kwa Marekani, Ulaya, China na Urusi.