1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger, Mali, Burkina Faso zaunda kikosi cha kukabili uasi

Sylvia Mwehozi
7 Machi 2024

Watawala wa kijeshi wa Niger, Mali na Burkina Faso wametangaza kuunda kikosi cha pamoja cha kupambana na wanamgambo wa itikadi kali katika nchi hizo.

https://p.dw.com/p/4dFIl
 Assimi Goïta, Abdourahamane Tiani, Ibrahim Traoré
Viongozi wa Mali, Niger, Burkina Faso Picha: Francis Kokoroko/REUTERS; ORTN - Télé Sahel/AFP/Getty; Mikhail Metzel/TASS/picture alliance

Watawala wa kijeshi wa Niger, Mali na Burkina Faso wametangaza kuunda kikosi cha pamoja cha kupambana na wanamgambo wa itikadi kali katika nchi hizo.

Mkuu wa jeshi wa Niger Moussa Salaou Barmou, amesema katika taarifa yake baada ya mazungumzo ya mjini Niamey kwamba kikosi hicho kipya kitaanza kufanya kazi hivi karibuni, haswa kushughulikia changamoto za kiusalama.

Soma: ECOWAS yaziondolea vikwazo Guinea, Mali

Ukubwa wa kikosi hicho haukuwekwa wazi, lakini kwa mujibu wa Barmou, majeshi ya nchi hizo tatu yamekubaliana kuunda wazo la opareisheni, itakayowaruhusu kufanikisha malengo ya usalama na ulinzi.

Tangazo hilo linazidi kuwaleta karibu majirani hao watatu ambao wamempiga kumbo mkoloni wa zamani na mshirika wa kijadi wa kiusalama, Ufaransa na kuigeukia Urusi.

Nchi zote tatu pia zilitangaza dhamira ya kujiondoa kwenye jumuiya ya ushirikiano wa kikanda ya ECOWAS.