SiasaNicaragua
Nicaragua yamwaachia huru Askofu mashuhuri wa kikatoliki
15 Januari 2024Matangazo
Askofu Rolando Alvarez na makasisi hao 18 walihukumiwa kifungo gerezani zaidi ya mwaka mmoja uliopita katika mfululizo wa kesi inazoaminika zilikuwa na dhima ya kuwanyamazisha viongozi wa kidini na wanasiasa wa upinzani nchini Nicaragua.
Rais Ortega aliwatuhumu wote waliokamatwa na kufungwa jela-- ikiwemo Askofu Rolando-- kwamba walikuwa waungaji mkono maandamano wa makubwa ya umma yaliyofanyika mwaka 2018 akidai yalidhamiria kuipindua serikali yake.
Kwenye taarifa yake ya usiku wa kuamkia leo, serikali ya taifa hilo la Amerika ya Kati imetangaza kuwa Askofu Rolando na wenzake wengine wameachiwa na kukabidhiwa kwa mamlaka za makao makuu ya kanisa katoliki. Taarifa ya serikali imesema taratibu zinafanyika kuwasafirisha kwenda Vatican.