Ni Senegal na Algeria fainali ya AFCON
18 Julai 2019Kizazi cha dhahabu cha wachezaji wa Senegal kinataka kuandika historia katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika, Afcon leo jioni wakati watakapotiana kifuani na Algeria mjini Cairo.
Akiwa mchezaji wa kiungo Cisse alikuwa nahodha wa Senegal ambayo ilikuwa kizazi kikuu cha dhahabu, hadi sasa kikiwa ni kizazi ambacho kilifikia robo fainali ya kombe la dunia mwaka 2002 na kushindwa na Cameroon katika fainali ya mataifa ya Afrika katika mwaka huo kwa mikwaju ya penalti.
Cisse alikuwa wa mwisho kati ya wachezaji watatu wa Senegal kukosa penalti mjini Bamako mji mkuu wa Mali lakini ana matumaini makubwa ya kuepuka kurejewa kwa hali hiyo Ijumaa hii mjini Cairo.
"Nina waamini sana wachezaji wangu na nahisi kwamba wanataka kufanikisha kitu," Cisse ameuambia mtandao wa CAFOnline.com baada ya ushindi katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Tunisia.
"Kizazi hiki ni bora kuliko kile cha mwaka 2002. Wachezaji wangu wameniambia watakuwa wazuri zaidi kuliko sisi, na wameweza.
Wakiongozwa na Sadio Mane, ambaye ametawazwa hivi karibuni bingwa ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya Champions League akiwa na Liverpool , maendeleo yao nchini Misri hayajaanguka patupu.
Walihitaji ushindi dhidi ya Kenya kuweza kusonga mbele kutoka katika kundi C ambalo lilikuwa na Algeria, Tanzania na Kenya , baada ya hapo kabla kushindwa na wapinzani wao katika fainali hii Algeria na ushindi wao katika michezo minne imekuja kupitia dakika za nyongeza, goli la kujifunga baada ya pande zote mbili kukosa penalti katika dakika za mwisho katika wakati wa kawaida.
"Haya ni matunda ya matayarisho ya muda mrefu," alisema Cisse. Wachezaji hawa wamefanyakazi kwa nguvu kwa miaka mitano mizima na sasa tunapata matunda yake ya kazi yao ngumu."
Algeria na nyota wake
Cisse amekuwa kocha tangu mwaka 2015 na anasema mafanikio yake yanatokana na uhusiano wa karibu alionao na wachezaji, kama mlinzi wa Napoli Kalidou Kuolibaly ambaye alimshawishi kuingia katika kikosi cha Simba wa Teranga badala ya Ufaransa.
Algeria ina nyota wake pia wakubwa katika ligi, sio mwingine zaidi ya mchezaji mahiri wa kati Riyad Mahrez wa mabingwa wa mataji matatu nchini Uingereza katika msimu mmoja manchester City.
Mahrez alifunga mkwaju wa dakika za mwisho na kuishinda Nigeria kwa mabao 2-1 katika mchezo wao wa nusu fainali , na kuzusha shangwe na hoi hoi uwanjani na pia Ufaransa, ambako mamia ya mashabiki walikamatwa wakati sherehe zilipofikia hatua ya kutoweza kudhibitiwa.
"Tumekuwa vizuri sana katika mashindano haya," Mahrez amesema. "Tumefunga mabao 12 na kufungwa mawili tu, lakini mchezo huu umetupa hali ya kujiamini zaidi kucheza fainali.
"Tuna uwezo wa kushinda."
Hali ya wasi wasi
Ushindi utaipa Algeria ushindi wake wa pili wa AFCON baada ya ule wa mwaka 1990, ambao ni pamoja na ushindi wa michezo minne dhidi ya Senegal.
"Tumecheza na Senegal katika awamu ya makundi na tunafahamu kuwa ni timu nzuri sana," amesema Mahrez. "itakuwa fainali ngumu. Lakini Senegal , tunafahamu nguvu zao na udhaifu wao na tutaingia uwanjani kuwapa mchezo mzuri."
Hali ya wasi wasi hata hivyo imehamia Ufaransa kuhusiana na mchezo huo wa fainali ya AFCON na sio mjini Algiers ama Dakar.
Polisi itaweka vikosi vyake usiku wa leo Ijumaa mjini Paris kuhakikisha usalama kwa ajili ya fainali za kombe la mataifa la Afrika, ambapo Senegal inacheza na Algeria. Polisi 2,500 watawekwa Ijumaa usiku mjini Paris kuhakikisha usalama katika eneo la Champs-Elysee kwa ajili ya fainali hiyo.
sherehe za ghasia zilizuka siku ya Jumapili nchini Ufaransa, ambako wanaishi jamii kubwa ya watu wenye asili ya Algeria , baada ya Algeria kuishinda Nigeria kwa mabao 2-1. Polisi ya Ufaransa iliwatia nguvuni zaidi ya watu 200.