1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu: Hatua za Israel zimesaidia anguko la Assad Syria

9 Desemba 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuanguka kwa Bashar al-Assad nchini Syria, ni matokeo ya moja kwa moja ya hatua za Israel katika eneo la Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/4ntpk
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Pool European Pressphoto Agency/AP/dpa/picture alliance

Netanyahu amsema matokeo hayo ni pamoja na pigo iliyopata Iran na Hezbollah ambao walikuwa washirika wakuu wa Assad.

Wachambuzi na watafiti wa masuala ya usalama wamesema kauli ya Netanyahu ina ukweli kwa kiasi fulani, ingawa kuanguka kwa Assad haikuwa mkakati wa Israel na ni tukio ambalo halikutarajiwa. Wameendelea kuwa, Urusi mshirika mkubwa wa Assad, imeelekeza nguvu zake katika vita vya Ukraine.

Netanyahu alimuonya Assad mnamo Novemba 27, siku ambayo waasi wa Syria yalianza mashambulizi yao,  na kumueleza kuwa alikuwa "akicheza na moto" kwa kuliunga mkono kundi la Hezbollah na kusaidia kusafirisha silaha hadi nchini Lebanon.