1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Hofu ya uwezekano wa kutofikiwa mapatano juu ya vita Gaza

3 Septemba 2024

Wasiwasi umeongezeka juu ya uwezekano wa kufikiwa mapatano ya kusimamisha mapigano Ukanda wa Gaza baada ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kukataa mwafaka kwenye mazungumzo kuhusu kuachiwa mateka wa Israel.

https://p.dw.com/p/4kERz
Israel | Maandamano | Benjamin Netanyahu
Raia wa Israeli wakusanyika kwa maandamano, wakitaka makubaliano ya kubadilishana mateka na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza, uchaguzi wa haraka na kusitishwa kwa mapigano. Picha: Mostafa Alkharouf/Anadolu/picture alliance

Netanyahu amewaambia waandishi wa habari baada ya kumalizika maandamano yaliyofanyika nchini Israel kote, kwamba hatakubali kushinikizwa ili arudi nyuma katika msimamo wa kufanya mazungumzo na Hamas juu ya  kuvimaliza vita.

Soma pia: Biden asema Netanyahu anakwamisha mapatano Gaza 

Baada ya kuuawa mateka sita kwenye Ukanda wa Gaza watu nchini Israel kote walifanya maandamano makubwa ya kuishinikiza serikali iwakomboe mateka waliobakia.

Rais wa Marekani Joe Biden alipokutana na wajumbe wa nchi yake wanaofanya mazungumzo na wajumbe wa Qatar na Misri kwa lengo la kuleta mapatano yatakayowezesha kuachiwa kwa mateka wa Israel waliobakia amesema Netanyahu hajachukua hatua za kutosha ili mateka waachiwe.