Netanyahu apinga kuipa mamlaka ya Palestina udhibiti Gaza
20 Januari 2024Katika mazungumzo yake na Biden, Netanyahu amesisitiza kuwa baada ya Hamas kuangamizwa, Israel inapaswa kuwa na udhibiti wa Gaza ili kuhakikisha kwamba eneo hilo halitakuwa tishio tena kwa Israel, suala ambalo linakwenda kinyume na matakwa ya mamlaka ya Palestina.
Viongozi hao wawili walizungumza kwa njia ya simu siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza katika muda wa karibu mwezi mmoja huku Biden akieleza kuwa, bado anaamini kuwepo kwa uwezekano wa Netanyahu kukubali kuundwa kwa taifa la Palestina.
Hata hivyo, afisa mkuu wa Hamas Izzat al-Rishq amepuzilia mbali kauli ya Biden juu ya uwezekano wa Israel kukubali kuundwa kwa taifa la Palestina.
Afisa huyo amesema Biden ni mshirika kamili wa mauaji ya Wapalestina na kwamba hawataraji lolote jema kutoka kwake.