Netanyahu akosoa uamuzi wa ICJ akisema uamuzi wa uwongo
20 Julai 2024Matangazo
Netanyahu ameonekana kuongoza kupaza sauti ya kulaani uamuzi wa mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa kuanzia kwa wanasiasa wa kihafidhina, wa siasa kali za mrengo wa kulia na hata walio na misimamo mikali nchini mwake.
Waziri huyo amesema Wayahudi sio walowezi katika ardhi yao, mahakama ya The Hague inapotosha ukweli wa kihistoria.
Wengine waliopinga uamzi huo wa Ijumaa ni pamoja na Itamar Ben Gvir, waziri wa usalama wa taifa wa mrengo mkali wa kulia,Waziri wa Fedha wa mrengo wa kulia Bezalel Smotrich ambae alitoa wito wa kunyakuliwa kwa Ukingo wa Magharibi kupita ukurasa wake wa X. Na Kiongozi wa upinzani wa Yair Lapid.