Ndege ya kuwaokoa watalii yatua New Caledonia
21 Mei 2024Hii ni safari ya kwanza ya uokoaji tangu uporaji, machafuko na milio ya risasi ilipoligubika eneo hilo ambalo ni himaya ya Ufaransa katika bahari ya Pasifiki siku nane zilizopita.
Australia na New Zealand zimetuma ndege za kwanza kwenda katika uwanja wa ndege wa Nourmea Magenta ambako waandishi wa shirika la habari la AFP wameshuhudia ndege ya kwanza ya Australia chapa C-130 Hercules ikitua na watalaii kadhaa wakisubiri.
Waziri wa mambo ya nje wa Australia Penny Wong amesema abiria wanaorodheshwa na kusafirishwa kulingana na mahitaji na wanaendelea kuratibu safari zaidi za ndege.
Waziri wa mambo ya nje wa New Zealnd Winston Peters amesema nchi yake inatuma ndege moja ya kijeshi kuwaokoa abiria 50 wenye mahitaji muhimu ya dharura kuwarejesha Auckland.