SiasaUkraine
Nchi za Magharibi wameahidi kuipa Ukraine makombora
4 Februari 2023Matangazo
Tangazo hilo lilijiri muda mfupi baada ya Zelensky kuuambia mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Kyiv kuwa hakuna atakayeusalimisha mji wa Bakhmut, akiapa kuwa watapigana kadri watakavyoweza.
Marekani imetangaza mpango mpya wa dola bilioni 2.2 wa silaha, ambao wizara ya ulinzi imesema zinajumuisha bomu jipya la usahihi linalofyatuliwa na kombora, ambalo linaweza kuongeza maradufu uwezo wa mashambulizi ya Kyiv dhidi ya wanajeshi wa Urusi. Ufaransa na Italia zitatoa mifumo ya makombora ya kufyatuliwa kutokea ardhini kwenda angani ambayo ni ya masafa ya wastani. Makombora hayo yanatoa ulinzi wa mashambulizi ya kutokea angani ama kutoka kwenye makombora au ndege za kivita.