Nchi za G7 zalaani ushirikiano wa Korea Kazkazini na Urusi
6 Novemba 2024Matangazo
Katika taarifa ya pamoja, wanadiplomasia hao walielezea wasiwasi wao kuhusu kupelekwa kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi, huku kukiwa na uwezekano wa kutumika kwa wanajeshi hao katika uwanja wa vita nchini Ukraine.
Viongozi wa G7 wakamilisha mkopo wa Ukraine uliotokana na mali za Urusi
Taarifa hiyo imeongeza kuwa uungaji mkono wa moja kwa moja wa Pyongyang katika vita vya uchokozi vya Urusi dhidi ya Ukraine, mbali na kuonyesha juhudi za kukata tamaa za Urusi kufidia hasara zake, utaashiria kutanuka kwa mzozo huo na kusababisha athari kubwa kwa amani na usalama wa Ulaya na eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki.
Taarifa hiyo ilitiwa saini na nchi za G7 pamoja na Australia, Korea Kusini, New Zealand na mjumbe mkuu wa Umoja wa Ulaya.