Afrika kufikiria kuwekeza katika mipango ya mazingira
21 Machi 2023Matangazo
Uamuzi wa nchi hizo masikini ambazo pia zinazongwa na madeni na hasara iliyosababishwa na uharibifu kutokana na matukio ya vimbunga, ukame na joto kali zimekubaliana hilo katika mkutano wa mawaziri wa fedha uliofanyika Addis Ababa siku ya Jumatatu.
Hatua hiyo itazifanya nchi masikini kupunguziwa madeni yake na badala yake nchi hizo za Afrika zitahitajika kuahidi kuwekeza katika mazingira.
Waziri wa fedha wa Misri Mohammed Maait amesema kwamba nchi yake ni moja kati ya nchi nyingi ambazo hivi sasa zinalazimika kuongeza fedha nyingi katika bajeti yake ya mazingira ambayo imepunguwa kwa kiasi kikubwa kutokana na madeni ya nje.