Nchi wanachama EAC wajadili soko la pamoja
21 Julai 2022Kikao hicho cha siku mbili kinajadili utekelezwaji wa itifaki ya soko huria na unafuu wa kufanya biashara, ambao kwa hivi siku za karibuni kumekuwa na malalamiko miongoni mwa nchi wananchama.
Mwenyekiti wa jumuia hiyo ambae pia ni rais wa Kenya Uhuru Kenyatta am,euwambia mkutano huo kwamba kuna haja sasa kama wananchama kujiuliza endapo bidhaa za nchi hizo kutouzika nje ya jumuia.
Soma pia:Ujerumani yatoa Euro 29 milioni EAC
Maetoa wito kwa kila nchi mwananchama kuhakikisha wanajitahidi katika kutataua changamoto ambazo moja kwa moja zimekuwa ni sababu ya mkwamo wa kulifikia soko la pamoja la EAC.
"tunajitahidi kama nchi moja moja na ndiyo maana kule Kenya tumejitahidi kujenga miundombinu"
Alisema rais Kenyatta akitolea mfano wa taifa lake na baadhi ya mataifa ndani ya jumuia ambayo yameonesha jitihada katika kukabiliana na changamoto zinazosababisha kutolifikia soko la jumuiya.
Kenya na Tanzania zasisitiza Afrika ijikite katika uzalishaji
Rais Kenyata akihutubia mkutano huo wa 22 wa jumuiya uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 300 kutoka nchi mbali mbali duniani, ametupa lawama kwa wale aliowataja kama wasiopenda maendeleo ya jumuiya ya Afrika mashariki, akisema wamekuwa wakiingilia mchakato wa maendeleo ya nchi hizo hukuwakinuia kuzifanya nchi za jumuiyahiyo kuwa masoko yao.
Ametilia msisitizo wa Waafrika kuzilisha bidhaa zao zenye ubora, kuuza ndani ya masoko yao na kutafuta masoko ya nje, tofauti na ilivyo sasa ambapo nchi nyingi za Afrika zinategemea bidhaa kutoka mataifa mengine wakati zinauwezo wa kuzalisha.
Kwa upande mwingine Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiongelea kama Afrika Mashariki inaweza kuwa na chakula cha kutosha bila kutegemea mataifa ya nje, amesema inawezekana kwa sababu kuna eneo kubwa la ardhi, lakini kinachohitajika ni uimarishwaji wa pembejeo za kilimo pamoja na kuimarisha mifumo ya kilimo cha umwagiliaji.
Soma pia:Viongozi wa EAC wakutana kujadili usalama wa Kongo
Rais Samia akizungumzia rasilimali ambazo zipo Afrika amesema ikiwemo mito na maziwa vitumike katika kuhakikisha kilimo kinaimarika na kuwa na chakula cha kutosha kwa misimu yotze ya kilimo.
"Ardhi inaweza kuwepo lakini tunahitaji pia kuangalia suala la umwagiliaji ili tuweze kupata tija ya kilimo katika misimu miwili au mwaka mzima" alisema rais Samia na kuoneza kwamba lazima kuwe na mfumo madhubuti wa kuhifadhi chakula.
"Tunatakiwa pia kuwa maghala ya kutunzia mavuno yetu na haya si lazima yawe ya kisasa ila hata yale yetu ya asili yanaweza kuboreshwa ili tuhifadhi chakula kwa ajili ya kujitosheleza kwa chakula'' aliongeza rais Samia.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Marais wa nchi za Kenya, Tanzania, Uganda na Somalia kama nchi mwalikwa, na nchi zingine ambazo ni Sudan Kusini, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na Rwanda wakituma wawakilishi.
Kikao cha Marais kitaendelea tena Kesho ijumaa ambapo wanatarajiwa kuteua majaji wa mahakama ya jumiya ya Afrika Mashariki, pamoja na kuzindua barabara ya mzunguko inayoziunganisha nchi za Keya na Tanzania.