1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi fadhili zaiahidi Liberia Dolla miliyoni 520

7 Februari 2004
https://p.dw.com/p/CFh4
NEW YORK: Mkutano wa kimataifa wa nchi fadhili kuhusu ukarabati wa Liberia iliyokumbwa na balaa la vita vya ndani, umemalizika kwa kuahidiwa nchi hiyo msaada wa Dollar miliyoni 520. Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan aliita jamii ya kimataifa kuipatia Liberia msaada wa alau Dollar miliyoni 500. Kwa kufuatana na tathmini ya Benki Kuu ya Dunia, mbali na zile Dollar miliyioni 170 zilizotolewa na UM kama msaada wa dharura wa kiutu, Liberia inahitaji Dollar nyingine miliyoni 488 mnamo miaka miwili ijayo ili kuukarabati uchumi wake. Mkutano huo wa nchi fadhili mjini New York ulihudhuriwa pia na Rais wa mpito wa Liberia Gyude Bryant.