1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaSyria

Nchi duniani kote zahamasisha misaada kwa Syria na Uturuki

7 Februari 2023

Nchi duniani kote zinahamasisha misaada ya haraka kwa ajili ya Syria na Uturuki ili ziweze kukabiliana na maafa yaliyosababishwa na mitetemeko ya ardhi ambapo watu zaidi ya 5000 wameshakufa.

https://p.dw.com/p/4NCF1
Srien Aleppo | Erdbeben
Picha: SNA/IMAGO

Nchi 19 za Umoja wa Ulaya zimeshakusanya vikosi vya madaktari na waokoaji 1500.  Ujerumani yenye watu wapatao milioni tatu wenye asili ya kituruki inaandaa kila aina za misaada.   Rais wa Marekani Joe Biden amesema vikosi vya waokoaji vya nchi hiyo vinafanya haraka ili kutoa misaada kwa waokoaji waUturuki.

Marekani imepeleka vikosi viwili vyenye jumla ya watu takriban 160. Kikosi cha waokoaji kutoka China tayari kimeanza kufanya kazi nchini Uturuki na pamoja na kikosi hicho China itatoa msaada wa haraka wa dola karibu milioni 6 kwa Uturuki kwa ajili ya mahitaji ya waokoaji. Rais wa Urusi Vladmir Putin pia ameahidi kupeleka vikosi vya waokoaji nchini Syria na Uturuki.

Wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema wananajeshi wa Urusi waliopo nchini Syria wanasaidia katika juhudi za uokozi. Uingereza pia imetangaza kuwa inapeleka waokoaji, vifaa pamoja na wataalamu. Nchi nyingine zilizoahidi kutoa misaada ni pamoja na Israel, Umoja wa Falme za Kiarabu,Ukraine, Japan, na India.