1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yairai Korea Kusini

30 Januari 2023

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO Jens Stoltenberg ameirai Korea Kusini leo kuongeza msaada wake wa kijeshi kwa Ukraine na kupendekeza taifa hilo litafakari sera yake ya kutopeleka silaha kwenye nchi zenye mizozo.

https://p.dw.com/p/4MrXP
Südkorea Seoul | Jens Stoltenberg trifft Verteidigungsminister Lee Jong-sup
Picha: Yonhap/picture alliance

Ametoa matamshi hayo baada ya kukutana na maafisa wa ngazi ya juu wa Korea Kusini mjini Seoul na kuwapatia mifano ya mataifa ikiwemo Ujerumani na Norway ambayo yamebadili sera zake za muda mrefu ili kuisaidaia Ukraine.

Stoltenberg yuko mjini Seoul, kituo cha kwanza cha ziara yake barani Asia itakayomfikisha pia nchini Japan, akilenga kutafuta uungaji mkono zaidi kwa mataifa washirika wa kanda hiyo katika kuukabili mzozo wa Ukraine na njia za kuidhibiti China.

Soma pia:NATO yadokeza kuipa Ukraine zana za nguvu zaidi

Korea Kusini ni muuzaji mkubwa wa silaha duniani lakini sera yake ya ulinziinapiga marufuku upelekeaji silahakwenye mataifa yenye vita.