NATO kuimarisha uhusiano wake na washirika wa Asia
11 Julai 2024Matangazo
Baada ya mkutano huo, viongozi hao pia watakutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, mwishoni mwa mkutano wa kilele wa NATO.
Mkutano kati ya viongozi wa nchi 32 wa NATO, Umoja wa Ulaya na wale wa kanda ya Bahari ya Hindi na Pasifiki ambazo ni Australia, Japan, New Zealand na Korea Kusini unatarajiwa kuangazia kitisho kinachowekwa na China na Urusi kwa kanda zote mbili.
Soma pia:Viongozi wa NATO wahitimisha mkutano wao wa kilele huko Marekani
Baadae macho yote yataelekezwa kwa Rais wa Marekani, Joe Biden, wakati akiufunga mkutano huo wa siku tatu uliogubikwa na mijadala ya masuala ya usalama na kusisitiza kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya uvamizi wa Urusi.