Mzozo kati ya Marekani na China unazidi kutokota. Kando na Marekani kutangaza vikwazo dhidi ya China, sasa nchi hiyo imeamuru pia ubalozi mdogo wa China mjini Houston ufungwe kwa madai ya ujasusi. China tayari imesema hatua hiyo ni uchokozi wa kisiasa utakaoathiri zaidi mahusiano yao kidiplomasia. Ahmed Rajab kutoka Uingereza anatoa tathmini yake.