1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Myanmar yasema imepoteza udhibiti wa mji wa kimkakati

2 Novemba 2023

China imetoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja Myanmar kaskazini, baada ya jeshi la nchi hiyo kusema limepoteza udhibiti wa mji wa kimkakati wa Chinshwehaw kaskazini mwa nchi hiyo katika mpaka na China

https://p.dw.com/p/4YJ73
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Wenbin
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Wenbin Picha: Kyodo/picture alliance

Haya yamesemwa na msemaji wa waziri wa mambo ya nje wa China Wang Wenbin aliyezitaka pande zinazozozana kusuluhisha tofauti zao kwa njia ya mazungumzo.

Katika taarifa, msemaji wa jeshi la Myanmar Zaw Min Tun ameyatuhumu makundi matatu yaliyojihami akisema yamelipua mitambo ya kuzalisha umeme, madaraja na kuharibu njia za usafiri.

Umoja wa Mataifa waunga mkono vikwazo dhidi ya Myanmar

Tangu Ijumaa iliyopita, kumekuwa na mapigano katika maeneo makubwa ya jimbo la kaskazini la Shan, ambako kunapangwa ujenzi wa njia ya reli yenye thamani ya dola bilioni moja, ikiwa ni sehemu ya mradi wa kimataifa wa China, wa ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa barabara na reli.