1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Myanmar yaingia mwaka wa 4 baada ya mapinduzi

1 Februari 2024

Uongozi wa kijeshi Myanmar umeonya kwamba utafanya "lolote lile" kuzima upinzani dhidi ya utawala wake.

https://p.dw.com/p/4buPY
Yangon, Myanmar | Mkuu wa Jeshi Min Aung Hlaing
Mkuu wa Jeshi Myanmar Min Aung Hlaing Picha: Aung Shine Oo/AP Photo/picture alliance

Haya yamesemwa na mkuu wa jeshi Min Aung Hlaing nchi hiyo ikiwa leo inaadhimisha mwaka wa nne tangu mapinduzi yaliyomuondoa madarakani kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasiaAung San Syu Kyi.

Tangazo hilo limekuja baada ya jeshi kuongeza muda wa hali ya dharura na kuchelewesha zaidi tarehe ya uchaguzi mpya ambao imeahidi kuufanya.

Soma pia:Myanmar yaamuru wafanyakazi kujiweka tayari kutumikia taifa

Upinzani wa utawala wa jeshi umezimwa katika maeneo ya mijini ila jeshi linapitia kipindi kigumu kuunyamazisha upinzani dhidi ya utawala wake katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Wiki hii, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa alisema hali ya haki za binadamu nchini Myanmar inazidi kuwa mbaya