1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurundi

Mwili wa rais wa zamani Burundi Buyoya warejeshwa nyumbani

17 Julai 2024

Mwili wa aliyekuwa rais wa Burundi Pierre Buyoya umerejeshwa nchini mwake ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu baada ya kuzikwa nchini Mali

https://p.dw.com/p/4iNrr
Rais wa zamani wa Burundi marehemu Pierre Buyoya
Buyoya aliishi Mali kwa miaka kadhaa akihudumu kama mjumbe maalum wa Umoja wa AfrikaPicha: STR/EPA/picture alliance

Mwili wa aliyekuwa rais wa Burundi Pierre Buyoya umerejeshwa nchini mwake, ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu baada ya kuzikwa nchini Mali alikoishi kwa miaka kadhaa kama mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika katika kanda ya Sahel.

Buyoya aliyefariki Desemba mwaka 2020 akiwa na umri wa miaka 71 mjini Paris kutokana na UVIKO-19,  alisifiwa kwa kusaidia kukuza demokrasia katika taifa hilo dogo la Afrika Mashariki, lakini alishutumiwa pia kwa kuwa na jukumu kubwa katika mauaji ya mrithi wake rais Melchior Ndadaye.

Afisa mwandamizi wa serikali ya Burundi alisema wakati huo kuwa Buyoya alikuwa na haki ya kuzikwa katika nchi yake lakini hatopewa mazishi ya heshima kama kiongozi wa zamani wa nchi kutokana na hukumu ya maisha jela iliyotolewa dhidi yake. Mabaki ya mwili wa Buyoya yatazikwa Jumatano huko Rutovu, kusini mwa Burundi.

Buyoya anatarajiwa kuzikwa leo 17.07.2024 nchini Burundi.