1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwili wa mateka wa Israel watambuliwa

10 Januari 2025

Mwili wa raia wa Israel aliyeshikiliwa mateka na wanamgambo huko Gaza tangu shambulizi la Oktoba 7, umetambuliwa baada ya mabaki yake kupatikana.

https://p.dw.com/p/4p1Bb
Israel Tel Aviv | Demonstration zur Freilassung der Hamas-Geiseln
Picha: JACK GUEZ/AFP

Kutokana na uchunguzi wa kitaalamu, jeshi la Israel limesema leo kuwa limeiarifu familia ya Hamza al-Zayadna kwamba aliuawa wakati akishikiliwa mateka na Hamas. 

Siku ya Jumatano, jeshi lilitangaza kuwa mwili wa baba yake, Hamza Youssef, uligunduliwa na ulirudishwa Israel. 

Soma pia:Vyanzo: Mashambulizi ya Israel yawaua zaidi ya watu 20 Gaza 

Wawili hao walikuwa sehemu ya mateka zaidi ya 200 waliochukuliwa na wanamgambo wa Kipalestina kutoka Kibbutz Holit karibu na mpaka wa Gaza, wakati wa shambulizi baya dhidi ya Israel, Oktoba 2023. 

Shambulizi la Hamas lilisababisha shambulizi la ulipizaji kisasi kutoka kwa Israel. Mapigano kati ya Israel na Hamas yamesababisha mauaji ya watu 46,000 huko Gaza, wengi wao wakiwa ni raia.