Mwenyekiti mpya wa Ukanda wa sarafu ya Euro
22 Januari 2013Mholanzi huyo anaechukua nafasi iliyoachwa wazi na Jean Claude Juncker alipingwa na Uhispania tu. Mwenyeketi huyo mpya Dijssebloem ameshaanza kazi yake licha ya upinzani wa Uhispania.
Mwenyekiti wa hapo awali Jean Claude Juncker aliwaambia waandishi wa habari mjini Burssels kwamba mawaziri wa fedha wa nchi za ukanda wa sarafu ya Euro wamemteua Dijsselbloem kuwa mwenyekiti wao. Uteuzi huo umekuja wakati wa kufaa kwa bwana Juncker alieuliza kwa mzaha jee nani atakuja kuniondoa mahala hapa?
Dijsselbloem atautumikia wadhifa wake mpya kwa muda wa miezi 30 lakini wakati huo huo ataendelea kuwa Waziri wa fedha wa nchi yake Uholanzi.
Mwenyekiti mpya ametoa mwito wa kufanya kazi zaidi ili kuudumisha mfumo wa kiuchumi na kijamii wa barani Ulaya unaothinimiwa sana. Amesema Ili kuweza kuudumisha mfumo huo inapasa kufanya kazi ili kuleta ustawi na kutenga nafasi mpya za ajira na wakati huo huo kuziweka bajeti sawa.Amesema malengo hayo yanaungwa mkono na mawaziri wa fedha wote wa jumuiya ya sarafu ya Euro.
Mwenyekiti mpya tayari atapigwa darubini kwenye mazungumzo ya mawaziri wa fedha kutoka nchi zote 27 za Umoja wa Ulaya mjini Brussels ambapo mawaziri hao watalijadili pendekezo la nchi 11 za ukanda wa Euro juu ya kuanzisha utaratibu wa kuzitoza kodi shughuli zote za kifedha.
Mwenyekiti mpya,Dijsselbloem wa kundi la nchi zinazotumia safaru ya Euro amesema kwake ni heshima kubwa kuchaguliwa kushika nafasi iliyoachwa wazi na Jean Claude Juncker. Dijsselbloem mwenye umri wa miaka 46 anachukua nafasi hiyo wakati ambapo nchi za kusini mwa Ulaya zimelemewa na mzigo wa madeni.
Waziri wa fedha wa Ufaransa Pierre Moscovici amesema anatummai kwamba Mwenyekiti mpya Jeroen Dijsselbloem ataleta urari katika jumuiya hiyo. Lakini hadi wiki iliyopita Ufaransa ilikuwa na mashaka juu ya mwenyekiti huyo mpya.Hatahivyo Waziri wa fedha wa Ufaransa Moscovici aliimpigia kura mholanzi huyo.
Waziri wa fedha wa a Ujerumani Wolfgang Schäuble amesema uteuzi wa Dijsselbloem ni jambo zuri wakati rais wa Baraza la Umoja wa a Ulaya Hermann Van Rompuy amesema viongozi wa nchi zote 17 za ukanda wa sarrafu ya Euro wanamuunga mkono. Hermann Van Rompuy amesema ana uhakika kwamba Dijsselbloem ndiye anaefaa.
Mwandishi:Hasselbach Christoph.
Tafsiri:Mtullya Abdu.
Mhariri:Josephat Charo