1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUbelgiji

Mustakabali wa waomba hifadhi Ulaya wajadiliwa Brussels

28 Septemba 2023

Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya wanakutaka mjini Brussels kujadili namna ya kuwashughulikia wahamiaji wanaowasili katika bara hilo kupitia njia ya bahari, wakati ongezeko la wahamiaji likizua hofu.

https://p.dw.com/p/4WuAJ
Belgien EU l Treffens der Außenminister der Europäischen Union in Brüssel
Moja ya mikutano ya mawaziri wa umoja wa ulaya mjini BrusselsPicha: Johanna Geron/REUTERS

Mawaziri hao watakuwa na nafasi nyengine ya kukubaliana juu ya mkakati uliokwama wa kugawana waomba hifadhi wanaofika Ulaya na kujadili pia iwapo Umoja huo ulio na wanachama 27 unaweza  kuingia katika makubaliano na Misri, kuwazuwia watu zaidi kuingia ulaya kupitia upande wa kusini wa bahari ya mediterenia.

Mwanadiplomasia mmoja wa Ulaya amesema kwa sasa kuna mivutano katika baadhi ya mataifa jirani ya Ulaya juu ya kuwepo au kutokuwepo makubaliano kama hayo, lakini akakiri kwamba mataifa mengi ya Ulaya yanataka hilo lifanyike.

Hata hivyo wakosoaji wanasema makubaliano kama hayo ya hivi karibuni yaliofanywa na Tunisia, yanakumbwa na ukiukaji wa haki za binaadamu, lakini kuna makubaliano mengine yanayotarajiwa kufanyika kwa sababu idadi  ya wahamiaji wanaowasili kupitia kisiwa cha Lampedusa  imeongezeka kuliko ile iliyoonekana mwaka 2022 wakati waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni aliposhinda uchaguzi mkuu kupitia suala hilo la uhamiaji.

Katika mkutano huu wa leo kipaumbele kipo kwa Ujerumani na iwapo waziri wa mambo ya ndani Nancy Faeser ataleta makubaliano ya pamoja mjini Brussels, yatakayoiruhusu Berlin kuunga mkono kile kinachojulikana kama "Mkakati wa Mgogoro" kitakachofungua njia ya kuwagawanya wakimbizi na wahamiaji katika mataifa ya Ulaya, ili kuepuka kuipa mzigo mkubwa Italia na mataifa mengine yanayokumbwa na kadhia ya wakimbizi.

Biashara haramu ya madawa ya kulevya ipo katika meza ya majadiliano.

Ecuador | Polizei stellt Kokain in Bananenkisten sicher
Polisi wa Equardo wakifanya upekuzi katika moja ya bandari nchini humo Picha: Marcos Pin/AFP/Getty Images

Awali waziri Faeser alitangaza ukaguzi wa mipaka ya Ujerumani na mataifa jirani ya Poland na Jamhuri ya Czech baada ya ujerumani kuona asilimia 80, ya ongezeko la waomba hifadhi mwaka huu jambo ambalo linatia wasiwasi, kwa  muungano wa mrengo wa kati kutoka kwa mrengo ya kulia katika chaguzi za ndani katika jimbo la Bavaria mwezi ujao.

Kwa upande wake rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, alitoa wito wa kufikiwa kwa makubaliano mepesi ya kisiasa kuelekea mabadiliko hayo ya mageuzi ya mfumo wa Umoja wa Ulaya kuhusu waomba hifadhi.

Kitu kingine kitakachojadiliwa kando na hili la wahamiaji ni mapambano  dhidi ya biashara haramu ya madawa ya kulevya kutoka Amerika ya kusini kuingia Umoja wa Ulaya. suala hilo litajadiliwa pamoja na wawakilishi wa maeneo husika.

Na suala jengine ambalo halina mjadala ni kurefusha muda wa kuwapokea wahamiaji wa Ukaine wanaoruhusiwa kuishi katika mataifa ya Ulaya bila ya kutuma maombi ya kuomba hifadhi. Mawaziri hao wanatarajiwa kurefusha muda huo hadi mwezi Machi mwaka 2025.

Chanzi: reuters/dpa