1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwandishi wa AFP auwawa Ukraine

10 Mei 2023

Shirika la Habari la Kimataifa la Ufaransa A FP limesema mwandishi wake Arman Soldin ameuwawa kwa shambulio la roketi karibu na mji wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4R7MX
Ukraine | AFP Journalist Arman Soldin
Picha: ARIS MESSINIS/AFP

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Shirika la Habari la Kimataifa la Ufaransa A FP limesema mratibu wake wa video wa Ukraine, Arman Soldin ameuwawa kwa shambulio la roketi karibu na mji wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine.

Baadae shirika hilo lilitoa taarifa yenye kusema mkasa huo ulitokea jioni ya Jumanne katika mji uitwao Chasiv Yar, ulio karibu na Bakhmut. Soldin alikuwa na umri wa miaka 32 na alizaliwa Sarajevo, eneo ambalo  kwa wakati huu ni mji mkuu wa Bosnia.

Vikosi vya Urusi vimekuwa vikijaribu kuuteka mji huo kwa muda wa miezi tisa, na hivyo kuufanya kuwa eneo la makabiliano ya kivita la muda mrefu zaidi nchini Ukraine.

Bakhmut katika kipindi cha makabiliano ya vita virefu zaidi. Itakumbukwa Mei 2022, mwandishi wa habari mwingine wa Ufaransa Frederic Leclerc-Imhoff, ambaye alikuwa kufanya kazi katika kituo cha televisheni cha Ukraine BFM-TV, aliuawa karibu mji wa Severodonetsk hukohuko mashariki mwa Ukraine.