SiasaIndia
Mwanasiasa wa India Baba Siddique auawa kwa kupigwa risasi
13 Oktoba 2024Matangazo
Baba Siddique, mwenye umri wa 66, na aliyehawi kuwa waziri katika jimbo la Maharashtra, alipigwa risasi kadhaa kifuani alipokuwa nje ya ofisi ya mwanawe mjini Mumbai jana usiku na alifariki dunia akiwa katika hospitali ya Lilavati jijini humo.
Siddique ambaye kwa miongo kadhaa alihusishwa na chama cha Indian National Congress alihamia hivi karibuni katika chama cha kikanda ambacho kinatawala Jimbo la Maharashtra linalotarajiwa kufanya uchaguzi mwezi Novemba.
Vyombo vya habari nchini India vimeripoti kuwa washambuliaji wawili wamekamatwa, na polisi bado inawamsaka mwingine mmoja. Washukiwa hao walidai kuwa sehemu ya genge la uhalifu ambalo limetekeleza mauaji mengi.