1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tola ashinda medali ya dhabau katika mbio za Marathon

10 Agosti 2024

Katika mashindano ya Olimpiki yanayoendelea mjini Paris, Ufaransa, mwanariadha wa Ethiopia Tamirat Tola ameshinda medali ya dhahabu katika mbio za Marathon kwa upande wa wanaume.

https://p.dw.com/p/4jKAB
Paris 2024 | Tamirat Tola
Tamirat Tola ameshinda medali ya dhahabu katika mbio za Marathon kwa upande wa wanaume.Picha: JOEL CARRETT/AAP/IMAGO

Tola alimaliza mbio hizo kwa muda wa saa mbili, dakika sita na sekunde 26, na kuwa mshindi wa kwanza wa Ethiopia wa mbio za Marathon upande wa wanaume ndani ya kipindi cha miaka 24.

Mkenya Eliud Kipchoge aliyetarajiwa kuweka historia kwa kushinda medali yake ya tatu ya dhahabu alishindwa kumaliza mbio, alijiondoa katika hatua ya kilomita 31 kutokana na kile klichoonekana kuwa maumivu. 

Uganda yashinda medali nyingine ya fedha ya Olimpiki

Bashir Abdi kutoka Ubelgiji alijinyakulia medali ya fedha akifanya vizuri zaidi baada ya kupata medali ya shaba katika michezo ya Tokyo huku Mkenya Benson Kipruto akipata medali ya shaba.