1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Mwanaharakati wa upinzani Urusi auawa katika uwanja wa vita

7 Oktoba 2024

Mwanaharakati Ildar Dadin ambaye alifungwa gerezani nchini Urusi kwa kuupinga utawala wa Rais Vladimir Putin, ameuawa katika uwanja wa vita katika mkoa wa alikokuwa akipigana kwa upande wa vikosi vya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4lTCL
Urusi | Vladimir Putin
Rais Vladimir PutinPicha: Kremlin.ru via REUTERS

Kifo chake kimethibitishwa na vyombo vya habari vya Urusi na familia yake jana Jumapili.

Dadin amesifiwa kama "mpiganaji jasiri na aliyejitolea kimasomaso” kupambana na Putin.

Soma pia: Urusi yaishambulia mikoa 15 ya Ukraine

Mwanaharakati huyo mwenye umri wa miaka 42 alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu gerezani mnamo mwaka 2015 kwa kuandaa maandamano dhidi ya mamlaka nchini Urusi.

Dadin alikuwa raia wa kwanza wa Urusi kuhukumiwa chini ya sheria ya mwaka 2014 inayozuia maandamano nchini humo.