1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Mwanaharakati wa Tunisia Khayam Turki akamatwa na polisi

11 Februari 2023

Polisi wa Tunisia wamemkamata mwanaharakati wa kisiasa, Khayam Turki na kumpeleka kusikojulikana. Hayo yameelezwa na wakili wake Abdelaziz Essid.

https://p.dw.com/p/4NN6Y
Tunesien Flagge auf dem Justizpalast in Tunis
Picha: Thierry Monasse/dpa/picture alliance

Turki, mwenye umri wa miaka 58, aliwahi kuzingatiwa kama mgombea angeliweza kuiongoza serikali baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Elyes Fakhfakh mnamo mwaka 2020, na ni mwanachama wa chama cha demokrasia ya kijamii cha Ettakatol.

Tunisia imeshuhudia ongezeko la kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa wanasiasa, waandishi wa habari na watu wengine tangu Rais Kais Saied kutwaa mamlaka muhimu katika hatua kali dhidi ya bunge mnamo Julai mwaka 2021. Tangu wakati huo, wapinzani wa Saied wamemtuhumu kwa ubabe.