1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati mshindi mbadala wa Tuzo ya Nobel

1 Oktoba 2020

Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Belarus, Ales Bialiatski Alhamis ametangazwa kuwa mmoja wa washindi wanne wa tuzo mbadala ya Nobel inayotolewa kila mwaka na wakfu wa Right Livelihood wa mjini Stockholm.

https://p.dw.com/p/3jH3n
SPERRFRIST 01.10.2020 / 9 Uhr MESZ / Right Livelihood Awards 2020, Ales Bialiatski, Belarus
Picha: HRC Vesna/Right Livelihood Awards 2020

Ales na shirika la haki za binadamu aliloasisi liitwalo Viasna wametambuliwa kwa mchango mkubwa wa kudai demokrasia na haki za binadamu nchini Belarus, ambako kwa wiki kadhaa waandamanaji wanapinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Agosti.

 Mshindi mwingine wa tuzo hiyo ni mwanasheria kutoka Iran Nasrin Sotoudeh aliyewatetea wanaharakati, wanasiasa wa upinzani na wanawake walioshtakiwa kwa kosa la kutovaa hijab.

 Washindi wengine wawili wa tuzo hiyo ni mwanasheria wa haki za kiraia wa nchini Marekani  Bryan Stevenson pamoja na mwanaharakati wa masuala ya mazingira kutoka nchini Nicaragua  Lottie Wren.