Mwanadiplomasia wa Misri afanya ziara ya kwanza Syria
27 Februari 2023Matangazo
Shoukry alifanya mazungumzo na Rais wa Syria Bashar Al-Assad pamoja na waziri mwenzake wa mambo ya nje Faisal Mekdad, na kusema amefikisha ujumbe wa mshikamano na huruma kwa niaba ya Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi.
Shoukry ndiye waziri wa tatu wa Kiarabu kukutana na Assad tangu tetemeko la Februari 6 lililozikumba Syria na nchi jirani ya Uturuki na kuuwa watu zaidi ya elfu 50, baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Jordan kutuma wanadiplomasia wao wa juu.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Misri pia anatarajiwa kufika nchini Uturuki, ambayo ilikuwa katika mzozo na Misri katika muongo uliyopita.