1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIran

Kifo cha binti wa Kiiran Mahsa Amini chatimiza mwaka mmoja

16 Septemba 2023

Raia nchini Iran wanaadhimisha leo mwaka mmoja tangu kilipotokea kifo cha Mahsa Amini, binti wa Kikurdi ambaye kifo chake kiliibua hasira na vuguvugu la maandamano kote nchini humo.

https://p.dw.com/p/4WPui
Maandamano ya kuipinga Iran nchini Uingereza
Kifo cha Mahsa Amini kilizusha wimbi kubwa la maandamano nchini Iran na maeneo mbalimbali dunianiPicha: Jonathan Brady/PA Wire/empics/picture alliance

Msichana huyo aliyekuwa na miaka 22 alikamatwa na polisi wa maadili kwa tuhuma za kukiuka kanuni za mavazi za Kiislamu. Alifariki Septemba 16 katika mazingira ya kutatanisha akiwa chini ya mikono ya polisi.

Ingawa hii leo hakuna miito ya maandamano nchini Iran kuadhimisha mwaka mmoja wa kifo cha Amini, wakazi wa jamii ya Kikurdi wanapanga kufanya kumbukumbu hiyo kwa kufunga maduka ili kuonesha mshikamano.

Ripoti zinasema vikosi vya ulinzi na vya kijeshi vimepelekwa kwenye mji alikozaliwa wa Saghes na mapema hii leo kulitolewa ripoti kwamba Baba wa Binti huyo alikamatwa kwa muda na maafisa wa usalama na kisha kuachiwa.