Mwaka mmoja wa vita Sudan: Hali inazidi kuwa mbaya zaidi
15 Aprili 2024Umoja wa Mataifa umesema mwaka mmoja wa vita vya Sudan kati ya majenerali hasimu nchini humo umesababisha maafa makubwa, mamilioni ya watu wakiyakimbia makazi yao huku wakikabiliwa na njaa na madhila mengine chungu nzima. Ripoti ya umoja wa Mataifa inasema upande wa kaskazini wa nchi hiyo ndio umeathirika zaidi na ndiko yanakoshuhudiwa maafa mabaya zaidi ya kibinadamu.
Soma zaidi.Wakimbizi wa Sudan wateseka Sudan Kusini
Kwa mujibu wa msemaji wa Shirika la Afya Ulimwenguni,WHO, Christian Lindmeier akizungumza mbele ya waandishi wa habari mjini Geneva amesema bila kusitishwa kwa mapigano nchini Sudan hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa siku zijazo na pia upo uwezekano kwamba athari zake zikasambaa hata kwa mataifa jirani.
Vita hivyo ambavyo vinatimiza mwaka mmoja tangu vilipozuka vimesababisha mamilioni ya wasudan kuwa wakimbizi huku wakikakabiliwa na ukosefu wa huduma za kimsingi ikiwemo chakula, kuharibika kwa miundombinu na kuenea kwa magonjwa ni miogoni mwa madhila wanayokumbana nayo kila siku.
Soma zaidi. Watu 12 wauawa katika shambulizi la droni nchini Sudan
Shirika la Afya Duniani linaeleza kuwa vita hivyo vimewaua maelfu ya watu na kusababisha maafa makubwa ya kibinadamu, Zaidi ya watu milioni 8.5 wamekimbia makazi yao, huku karibu milioni 1.8 wakivuka mipaka ya nchi hiyo kwenda kwenye mataifa mengine.
WHO yaendelea kutoa onyo kwa jumuiya ya kimataifa
WHO imeonya kuhusu kudorora kwa mfumo wa afya, uhaba wa wafanyakazi. dawam, chanjo na vifaa vya afya, asilimia 70 hadi 80 ya vituo vya afya vya Sudan havifanyi kazi kutokana na mapigano hayo yanayoendelea.
Balozi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield amesema wakati jamii zikukubana na njaa, magonjwa nayo yanazidi kuhatarisha usalama wa maisha yao.
"Wakati jamii zikikabiliana na njaa, ugonjwa wa kipindupindu na surua unazidi kuenea, huku ghasia zikiendelea kugharimu maisha ya watu wengi, dunia kwa kiasi kikubwa imekaa kimya, na hilo lazima libadilike. Na lazima libadilike sasa. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kutoa zaidi. Ni lazima kufanya hivyo. zaidi. Na inapaswa kujali zaidi."amesema balozi huyo.
Soma zaidi. Shule zitafunguliwa tena Sudan Kusini baada ya wiki mbili za joto kali
Kwa sasa vikosi vya Shule zitafunguliwa tena Sudan Kusini baada ya wiki mbili za joto kali serikali nchini Sudan vinatumia nguvu kubwa ya mashambulizi ya anga kuyarudisha maeneo ambayo yamechukuliwa na kikosi cha RSF ingawa upo ukosoaji kwamba jeshi hilo limeshindwa kuwalinda raia wakati wa mashambulizi yake.
Utafiti wa Umoja wa Mataifa unaonyesha kuwa mwaka 2024 utakuwa mwaka wa njaa zaidi nchini Sudan hasa katika miji ya Darfur na Kordofan na hiyo ni kutokana na kupoungua kwa uzalishaji na mfumuko mkubwa wa bei.
Kongamano la kimataifa la kibinadamu kwa ajili ya Sudan likiongozwa na Ufaransa liaandaa mkutano mjini Paris wa kujadili namna ya kuongeza ufadhili huku asilimia sita tu ya makadirio ya dola bilioni 2.7 zinazohitajika kushughulikia mzozo huo zikiwa zimekusanywa hadi sasa.