Mwaka 2024 kuwa mwaka wenye joto zaidi
9 Desemba 2024Matangazo
Kiwango hicho kipya kilichothibitishwa na shirika hilo la Copernicus, kinahitimisha mwaka ambapo nchi tajiri na maskini zilikumbwa na majanga ambayo wanasayansi wamehusisha na shughuli za binadamu katika ongezeko la kasi la joto duniani.
Copernicus inasema, hali ya joto isiyo ya kawaida iliongeza kiwango cha wastani cha halijoto duniani kati ya Januari na Novemba hivi kwamba mwaka huu ulikuwa na uhakika wa kuwa na viwango vya juu vya joto visivyo vya kawaida.
Katika hatua nyingine mbaya, 2024 utakuwa mwaka wa kwanza wa joto la zaidi ya nyuzi 1.5 kuliko nyakati za kabla ya viwanda kabla ya wanadamu kuanza kuchoma kiasi kikubwa cha nishati ya visukuku.