Mvutano wa kisiasa Madagascar
27 Mei 2009Rais mpya wa Madagascar amemkatalia ruhusa ya kurejea nyumbani kutoka uhamishoni,rais aliyepinduliwa Marc Ravalomanana.Kwa kufanya hivyo Andry Rajoelina amevuruga juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo wa kisiasa kisiwani Madagascar..
Andry Rajoelina ametoa amri hiyo siku moja baada ya Ravalomanana kumtuhumu anashirikiana na dola kuu la zamani la kikoloni Ufaransa ili kuwageuza watumwa wananchi wa Madagascar.
Mazungumzo yanayozileta pamoja pande zote za kisiasa,yanayofuatiliziwa kwa makini na madola ya kigeni na wateja katika kisiwa hicho cha bahari ya Hindi chenye utajiri wa maadini yanayotarajiwa kurejewa leo.
Washirika wa Ravalomanana anaeishi uhamishoni nchini Afrika kusini,wamearifu kwam,ba watasusia mazungumzo zaidi ikiwa mazungumzo ya kurejea haraka kwa Ravalomanana hayataanza haraka.
"MMamlaka makuu ya mpito yanazuwia kurejea kwa Marc Ravalomanana nchini"-Rajoelina aliwaambia maripota wakati yakifumnuliwa mazungumzo tofauti yenye shabaha ya kuondoa tofauti jeshini.
Jana jioni ,rais wa zamani Ravalomanana, aliituhumu Ufaransa kuwaungamkono viongozi wa njama ya mapinduzi kisiwani Madagascar na kuwa inatumikia tu masilahi yake kisiwani humo.Washirika wa Ravalomanana wakidaikuna mkono wa Ufaransa katika kuingia madarakani kwa Rajoelina,meya wa zamani wa Antananarivo.Lakini hii ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa msukosuko wa kisiasa kisiwani humo, wanainyoshea Ufaransa kidole moja kwa moja.
rais huyo wa zamani Ravalomanana aliacha madaraka baada ya kutiwa shinikizo kubwa na wafuasi wa kundi la Rajoelina akisaidiwa na wanajeshi walioasi.Msukosuko wa kisiwa hiki ukachafua biashara ya utalii yenye kukipatia kisiwa hiki dala milioni 390 kwa mwaka.
"Azma ya Ufaransa ni kuirejesha Madagaskar katika ukoloni wake na kuwageuza tena watu wake watumwa.Azma yao ni kuzusha vita vya kikabila." Rais huyo wa zamani alisema akiwa Afrika kusini uhamishoni.
Akaongeza kusema kwamba, Ufaransa haitaki kuiona Madagascar inaebdelea ,bali inatetea mno masilahi yake tu.
Mapatano ya kukomesha vurzgu kisiwani Madagascar yalibainika kukaribia kufikiwa ijumaa iliopita pale mjumbe wa UM aliposema pande zinazogombana zimeafikiana kuunda serikali ya aina ya umoja wa Taifa.Lakini siku iliofuatia, ujumbe mmoja ukajitoa kwenye mazungumzo na ujumbe wa Ravalomanana ukasema nao utafuata njia hiyo ya kujitoa ikiwa hakutapatikana maafikiano juu ya kurejea kwake nchini.
Ravalomanana anaedai kuwa bado yeye ni kiongozi halali wa Madagascar,alikuwa na uhusiano wa mvutano na Ufaransa.Alimtimua balozi wa Ufaransa Gildas Le Lidec,Julai mwaka jana baada ya kuwapo kisiwani miezi michache tu.
Balozi mpya aliwasili siku chache tu baada ya mageuzi ya utawala ya Machi,mwaka huu lakini, hakuanza bado rasmi kazi zake.Rais Nicholas Sarkozy, ni miongoni mwa viongozi wa dola za kigeni na wale wa kimkoa waliomtuhumu Meya huyo wa zamani wa Antannanarivo-mpiga Disco kupanga ile njama ya mapinduzi.
Muandishi: Ramadhan Ali /RTRE
Mhariri:M-Abdulrahaman