1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvua yauwa watu 49 nchini India

14 Agosti 2023

Mafuriko nchini India yamesababisha,vifo vya takriban watu 49, tisa kati yao wamepoteza maisha kufuatia kuporomoka kwa hekalu la ibada nchini humo,

https://p.dw.com/p/4V9BE
Indien | Starkregen im Himalaya
Picha: REUTERS

N watu wengine chungunzima inakhofiwa hawajulikani waliko baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko na maporomoka ya ardhi. Watu 41 wamepoteza maisha ndani ya kipindi cha masaa 24 katika mkoa wa Himachal Pradesh.Mvua za siku kadhaa zimesababisha mafuriko yaliyosomba magari,majumba kuporomoka na kuvunjika kwa madaraja katika majimbo ya kaskazini ya Uttarakhand na Himachal Pradesh. Hali ya mafuriko na maporomoko ya ardhi sio kitu kigeni katika maeneo hayo na husababisha uharibifu mkubwa katika msimu wa masika lakini wataalamu wanasema mabadiliko ya tabia nchi yameongeza kasi ya hali hiyo pamoja na athari.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW