Muungano wa upinzani wa Ujerumani wajadili tena uhamiaji
10 Septemba 2024Matangazo
Mkutano huo unaofanyika mjini Berlin ni wa pili katika awamu ya mazungumzo yanayovihusisha vyama tofauti, tangu kulipotokea shambulizi la kisu katika mji wa Sollingen mwezi uliopita na kurejesha masuala ya uhamiaji katika ajenda za kisiasa.
Mkutano huo wa ngazi ya juu kuhusu uhamiaji unalenga kufafanua mkakati wa pamoja wa serikali.
Muungano wa upinzani wa CDU/CSU umeitaka serikali ya Kansela Scholz inayoongozwa na chama cha siasa za wastani za mrengo wa shoto, kuanzisha hatua kali za kukabiliana na wahamiaji katika mipaka ya Ujerumani.
Hilo lilikuwa sharti la awali la kuendelea na mazungumzo zaidi.