1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musk atoa dola milioni 44 kumsaidia Trump kwenye kampeni

Angela Mdungu
25 Oktoba 2024

Bilionea na mwanzilishi wa jukwaa la SpaceX, Elon Musk ametoa jumla ya dola milioni 44 kwa kundi la America PAC linalofanya kampeni kwa niaba ya mgombea wa urais wa Marekani Donald Trump.

https://p.dw.com/p/4mEvY
Trump na Elon Musk
Elon Musk akizungumza jukwaani akiungana na Rais wa zamani wa Marekani na Donald Trump wakati wa mkutano wa kampeni Pennsylvania Oktoba 5, 2024.Picha: JIM WATSON/AFP

Taarifa hiyo iliyofichuliwa kutoka kwenye jalada la Tume ya taifa ya Uchaguzi, imeeleza kuwa fedha hizo zilitolewa mwanzoni hadi katikati ya mwezi huu wa Oktoba. Taarifa ya awali ilioonesha kwamba bilionea Musk, alitoa takriban dola bilioni 75 katika muda wa miezi mitatu, kwa makundi yanayomfanyia kampeni Donald Trump ikiwa ni juhudi zake za kumuunga mkono mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican kwenye uchaguzi wa Novemba 5. Mpaka sasa Kampeni ya Trump imetumia zaidi ya dola milioni 88 huku ya Kamala Harris ikitumia zaidi ya dola milioni 130 kufanya matangazo.