Museveni aapa kuwaandama waliouwa watalii, muongozaji wageni
19 Oktoba 2023Matangazo
Maafisa wa Uganda wamelishtumu kundi la waasi wa ADF kuwauwa wanandoa hao, ambo walikuwa raia wa Afrika Kusini na Uingereza pamoja na muongozaji wao raia wa Uganda, Jumanne jioni katika Mbuga ya Wanyama ya Malkia Elizabeth II.
Soma zaidi: Museveni alaani mauaji ya watalii
Kundi la ADF, ambalo lilianzisha uasi nchini Uganda na limekuwa likiendesha shughuli zake katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo tangu mwishoni mwa miaka ya 1990, lilitangaza utiifu kwa kundi la Dola la Kiislamu (IS) miaka minne iliyopita.
Soma zaidi: Mauaji ya watalii yazusha wasiwasi Uganda
Kundi la IS limedai kupitia chanaeli yake ya Telegram kuhusika na shambulio hilo la Jumanne.