Yunus atoa wito wa kuungana kuijenga upya Bangladesh
10 Agosti 2024Mama huyo alihuzunishwa na kisa cha mwanawe Abu Sayeed aliyeuwawa kwa kupigwa risasi katika maandamano makubwa yaliyohitimisha utawala wa miaka 15 wa Waziri Mkuu Sheikh Hasina.
Yunus ambaye ni mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel, alirejea nchini kutoka barani Ulaya alikokuwa uhamishoni, ili kuiongozi nchi yake kuelekea mageuzi ya kidemokrasia. Yunus amesema wajibu wake sasa ni kujenga Bangladesh mpya isiyokuwa na migawanyiko ya kidini.
Yunus asifu ´ukombozi wa pili´ wa Bangladesh
Kazi kubwa itakayomkabili Yunus kwa sasa ni kurejesha umoja na amani pamoja na kuingoza nchi hiyo katika kuandaa uchaguzi mpya baada ya kuondolewa kwa Hasina. Hata hivyo mtoto wa kiume wa Hasina, Sajeeb Wazed amesema serikali iliyoko sasa sio halali.
Serikali ya Sheikh Hasina aliye na miaka 76 inashutumiwa kwa matukio makubwa ya ukiukwaji wa haki za binaadamu ikiwemo mauaji ya kiholela ya maelfu ya wapinzani wake kisiasa. Hasina anasemekana kuitoroka nchi na kuimbilia nchini India.