Mtu mwenye uraia wa Iran na Sweden anyongwa Iran kwa ugaidi
6 Mei 2023Habib Chaab anadaiwa kuhusika na vifo vya watu kadhaa kwenye gwaride la kijeshi katika mji huo. Amenyongwa leo Jumamosi. Mtu huyo alikamatwa na majasusi wa Iran mnamo mwaka 2020 baada ya kuondoka Sweden na kwenda Uturuki ambako alikamatwa.
Soma zaidi:Ripoti: Idadi ya wanaonyongwa Iran yapanda kwa asilimia 25
Kesi iliyomkabili ilianza mnamo mwaka huo juu ya mashtaka ya kuongoza kundi la waasi. Alihukumiwa adhabu ya kifo mwezi Desemba mwaka uliopita. Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden, Tobias Billstrom ameelezea masikitiko yake kutokana na kunyongwa kwa Chaab, amesema serikali yake iliiomba Iran isiitekeleze adhabu hiyo. Billstrom, ambaye nchi yake kwa sasa inashikilia urais wa Umoja wa Ulaya amesema nchi zote za jumuiya hiyo ya Umoja wa Ulaya zimelaani kunyongwa Habibi Chaab.