MigogoroMashariki ya Kati
Mtu mmoja auwawa Israel kufuatia shambulizi la droni
19 Julai 2024Matangazo
Taarifa ya shambulio hilo imethibitishwa na afisa wa jeshi la Israel aliyekiri kuwa makosa ya kibinadamu, ndiyo sababu ya kushindwa kuizuia droni hiyo.
Kulingana na afisa huyo wa jeshi la Israel aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, droni yenye uwezo wa kusafiri masafa marefu ilishambulia majira ya saa tisa alfajiri.
Ameongeza kuwa, madhumuni makubwa ya shambulio hilo yalikuwa ni kuwauwa raia ndani ya Israel. Waasi wa Kihouthi wa Yemen wamethibitisha kuhusika na shambulio hilo.
Hayo yakijiri, bunge la Israel lilipiga kura jana kupinga taifa la Palestina linalochukuliwa kuwa kitisho, siku moja baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuwaambia wabunge kuwa jeshi limewakalia kooni wanamgambo wa Hamas.