AfyaAfrika Kusini
Mtu mmoja afariki dunia kufuatia homa ya nyani Afrika Kusini
12 Juni 2024Matangazo
Kulingana na waziri wa afya Joe Phaahla, visa hivyo vitano vilivyoripotiwa kati ya Mei 8 na Juni 7 ndivyo vya kwanza kurekodiwa nchini humo tangu mwaka 2022.
Homa ya nyani ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi na unasambazwa kupitia mawasiliano ya karibu na mtu au mnyama aliyeambukizwa.
Mwaka 2022, maambukizi ya ugonjwa huo yaliongezeka kote duniani, hasa miongoni mwa wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja hatua iliyopelekea Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO, kutangaza hali ya dharura duniani.
WHO ilitangaza mwisho wa hali hiyo ya dharura mwaka jana ila maambukizi ya machache yanaendelea chini kwa chini.