SiasaMarekani
Aliyemshambulia mume wa Nancy Pelosi ahukumiwa miaka 30 jela
18 Mei 2024Matangazo
David DePape alipatikana na hatia mwaka jana kwa kuingia kinyume cha sheria kwenye nyumba ya wanandoa hao mjini San Francisco na kumshambulia Paul Pelosi katika shambulio la kutisha lililonaswa na kamera za usalama.
Tukio hilo lilifanyika mnamo mwezi Oktoba mwaka 2022.
Awali, waendesha mashtaka walikuwa wameiomba mahakama ya shirikisho huko San Francisco kumhukumu DePape kifungo cha miaka 40 jela. Watu wengine ambao mshtakiwa huyo alikiri kutaka kuwashambulia ni pamoja na Gavana wa California Gavin Newsom, mtoto wa Rais Joe Biden - Hunter, na mwigizaji Tom Hanks.