1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mswada wa usalama Sudan Kusini sheria bila saini ya rais

16 Agosti 2024

Mswada tata wa usalama wa Sudan Kusini unaoruhusu kutiwa nguvuni kwa watu vila vibali rasmi vya kukamatwa, umekuwa sheria bila ya rais kuutia saini.

https://p.dw.com/p/4jXZ8
Salva Kiir Mayardit | sudanesischer Präsident
Picha: Samir Bol/ZUMAPRESS/picture alliance

Msemaji wa bunge Oliver Mori ameliambia shirika la habari la AP kuwa, mswada huo umekuwa sheria moja kwa moja kwa mujibu wa katiba kufuatia kupita kwa siku 30 tangu uwasilishwe kwa Rais Salva Kiir mnamo Julai 12.

Kiir hakuutia saini wala kuupinga mswada huo ambao umezua ukosoaji kutoka kwa wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na baadhi ya mataifa.

Mwezi uliopita, wajumbe tisa wa mataifa ya Magharibi, wakiwemo wawakilishi kutoka Marekani na Uingereza, walisema raia wa Sudan Kusini wanapaswa kuwa na haki ya kujieleza bila ya hofu ya kukamatwa kiholela au kutishwa na vikosi vya usalama.

Sudan Kusini inatarajiwa kufanya uchaguzi wake wa kwanza Disemba 22 chini ya serikali ya mpito iliyoundwa baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani mwaka 2018 na uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya karibu watu 40,000.