1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshirika wa Khamenei ajisajili kuwania urais Iran

1 Juni 2024

Kamanda wa zamani wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi ya Iran aliyeekewa vikwazo na Marekani Vahid Haghanian, ni miongoni mwa wagombea waliojisajili kugombea nafasi ya urais iliyowachwa wazi baada ya kifo cha Ebrahim Rais

https://p.dw.com/p/4gWwl
Iran Vahid Haghanian
Kamanda wa zamani wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi ya Iran Vahid Haghanian, ajisajili kugombea kiti cha uraisPicha: Mehr

Haghanian, ambaye ni mshirika wa karibu wa kiongozi wa juu ya Iran Ayatollah Ali Khamenei, aliwaambia waandishi habari baada ya kujisajili kwamba, anastahili kuwa katika nafasi hiyo hasa baada ya uzoefu wake wa miaka 45 katika ofisi ya rais na ya kiongozi mkuu.   

Spika wa zamani wa bunge Ali Larijani, Gavana wa zamani wa benki kuu nchini humo  Abdolnaser Hemmati ni miongoni mwa watu 12 waliojisajili kugombea nafasi hiyo. Hemmati amesema kikubwa atakachokifanya kipata nafasi hiyo ni kutumia diplomasia kuondoka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran na kuwa na mahusiano mema na nchi za nje.

Marekani yasusia kutoa heshima kwa hayati Raisi

"Juhudi zangu zote zitaelekezwa katika kufanya kazi na majirani zetu, kutanua ushirikiano wa kiuchumi na nchi zote zinazoweza kufanikisha masilahi yetu ya kitaifa. Nitatumia pia diplomasia kuondoa vikwazo na kuwa na mahusiano na ulimwengu wa nje," alisema Hemmati.

Baada ya usajili wagombea watachujwa na Baraza la viongozi wa kidini.